INJILI SONGS
Mteteeni Yesu
Mteteeni
Yesu, Mlio askari
Inueni
beramu, Mukae tayari
Kwenda
naye vitani, Sisi hatuchoki
Hata
washindwe pia, Yeye amiliki.
Mteteeni
Yesu, Vita ni vikali;
Leo siku
ya Bwana, Atashinda kweli
Waume
twende naye, Adui ni wengi,
Lakini
kwake Bwana, Tuna nguvu nyingi.
Mteteeni Yesu, Wenye ushujaa;
Nguvu zenu za mwili, Hazitatufaa;
Silaha
ya injili, Vaeni daima;
Kesheni
Mkiomba, Sirudini nyuma,
Mteteeni
Yesu, vita ni vikali
Wengi wamdharau, Hawamkubali;
Ila
atamiliki, Tusitie shaka;
Kuwa
naye vitani, Twashinda hakika
PANDA ASUBUHI
Panda asubuhi mbegu ya fadhili,
Panda
adhuhuri, tena jioni;
Tutaingojea siku ya mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno
Leta mavuno, leta mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno;
Leta mavuno, leta
mavuno
Tutafurahi kuleta mavuno.
Na panda mwangani, tena kivulini,
Usiwe na hofu kwa baridi mkuu;.
Na mwisho wa kazi kuvuna mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno.
Mvunieni Bwana kwa machozi mengi,
Ijapo twaona taabu nyingi; mwisho wa
Kiliyo tutakaribishwa
Tutafurahi kuleta mavuno
Comments
Post a Comment