Mteteeni Yesu Mteteeni Yesu, Mlio askari Inueni beramu, Mukae tayari Kwenda naye vitani, Sisi hatuchoki Hata washindwe pia, Yeye amiliki. Mteteeni Yesu, Vita ni vikali; Leo siku ya Bwana, Atashinda kweli Waume twende naye, Adui ni wengi, Lakini kwake Bwana, Tuna nguvu nyingi. Mteteeni Yesu, Wenye ushujaa; Nguvu zenu za mwili, Hazitatufaa; Silaha ya injili, Vaeni daima; Kesheni Mkiomba, Sirudini nyuma, Mteteeni Yesu, vita ni vikali Wengi wamdharau, Hawamkubali; Ila atamiliki, Tusitie shaka; Kuwa naye vitani, Twashinda hakika PANDA ASUBUHI Panda asubuhi mbegu ya fadhili , Panda adhuhuri, tena jioni; Tutaingojea siku ya mavuno, Tutafurahi kuleta mavuno Leta mavuno, leta mavuno, Tutafurahi kuleta mavuno; Leta mavuno, leta mavun...